Visima Kwanza ni kampuni inayoongoza katika sekta ya uchimbaji wa visima na utoaji wa suluhisho la miundombinu ya maji nchini Tanzania. Kwa miaka mingi, tumejenga sifa ya kutoa huduma bora na za kuaminika kwa wateja wa makazi, kilimo, viwanda na taasisi katika mikoa mbalimbali ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma, Arusha, Mwanza, Tabora, Shinyanga, Rukwa na Kilimanjaro. Huduma zetu ni pamoja na: Uchimbaji wa visima kwa kutumia mitambo ya kisasa Utafiti wa kijiofizikia (resistivity survey) kubaini eneo bora la kuchimba Ufungaji wa mabomba ya PVC na casing Ufungaji wa pampu za solar zinazotumia nishati ya jua Ujenzi wa minara ya matanki ya maji kwa ajili ya kuhifadhi na kusambaza maji Usafishaji wa visima vilivyoziba au kupungua ufanisi Upimaji wa ubora wa maji Ofisi yetu ipo Shoppers Plaza, Mikocheni, Dar es Salaam, na tunafanya kazi kote nchini Tanzania.
Business details are provided by the vendor. Confirm before visiting or paying.